
TABORA: Wananchi watakiwa kuwasaidia na kuwajali watu wenye ulemavu.
Wananchi mkoani TABORA wametakiwa kuwajali na kuwasaidia watu wenye ulemavu pindi wanapokuwa katika majukumu yao ya kila siku.
Wito huo umetolewa na mkuu wa wilaya ya TABORA,Mwalimu QUEEN MLOZI,wakati akizungumza katika hafla ya kuwakabidhi vifaa mbalimbali watu wenye walemavu katika viwanja vya Taasisi ya sanamu la Mwalimu NYERERE mjini TABORA
Vifaa hivyo vimetolewa na taasisi isiyo ya kiserikali ya Daktari AMONI MKOGA kwa kushirikiana na Ubalozi wa KUWAIT hapa nchini.
MLOZI pia amewasihi watu wenye ulemavu kuwa jasiri katika utendaji wa kazi zao badala ya kujishusha na kuonekana kama wametengwa na jamii jambo ambalo siyo kweli.
Mwenyekiti wa taasisi iliyotoa msaada kwa baadhi ya watu wenye ulemavu,Daktari AMONI MKOGA amesema taasisi yake imeamua kujikita kusaidia makundi maalumu baada ya kutambua makundi hayo yana uhitaji mkubwa wa msaada katika jamii.
Baadhi ya watu wenye ulemavu waliopata msaada ya baiskeli za kutembelea wamesema baskeli hizo zitawasaidia katika shughuli za mizunguko yao.
Naye mwananchi mmoja miongoni mwa waliohudhuria hafla hiyo mkazi wa kata ya MBUGANI,MAULIDI SHABANI ameipongeza taasisi ya Daktari,AMON MKOGA kwa kujitolea kuwasaidia makundi ya watu wenye ulemavu.
Taasisi ya Dkatari MKOGA kwa kushirikiana na ubalozi wa KUWAIT imetoa msaada wa baiskeli kwa walemavu wa miguu,fimbo za kutembelea kwa wenye uoni hafifu na cherehani za kushonea nguo kwa baadhi ya vikundi vya walemavu.