Skip to content
CGFM
  • Home
  • Listen Live
  • News
  • Presenters
  • Gallery
  • Advertise
Local

TANZIA: Mzee Kingunge Ngombale-Mwiru afariki dunia Tanzania

  • February 2, 2018February 2, 2018

Mwanasiasa mkongwe nchini Tanzania Kingunge Ngombale-Mwiru, 87, amefariki dunia. Mzee Kingunge amekuwa akitibiwa katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili.

Mwanasiasa huyo mkongwe alilazwa hospitalini mwanzoni mwa Januari akiuguza majeraha ya kushambuliwa na kung’atwa na mbwa nyumbani kwake na akafanyiwa upasuaji.

Alikuwa mmoja wa viongozi wa muda mrefu na miongoni wa watu waliokuwa na ushawishi katika Chama cha Mapinduzi (CCM) hadi alipojiuzulu kutoka kwenye chama hicho Oktoba 2015 akilalamikia alichosema ni ukiukaji wa katiba ya chama hicho.

Kabla ya kujiuzulu, alikuwa amesema kwamba hakuwa amefurahishwa na utaratibu uliotumiwa kumteua mgombea urais wa CCM mjini Dodome Julai mwaka huo.

Hata hivyo, aliahidi kutohamia chama kingine.

Bw Kingunge alikuwa amehudumu katika CCM tangu kuanzishwa kwa chama hicho mwaka 1977.

Mke wake, Peras, alifariki dunia mwezi uliopita akitibiwa pia Muhimbili baada ya kulazwa kwa miezi kadha.

Magufuli
Rais Magufuli alimjulia hali Mzee Kingunge alipolazwa hospitalini.

Rais wa Tanzania Dkt. John Magufuli alikuwa amefika katika Wodi ya Mwaisela iliyopo katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili kumjulia hali Mzee Kingunge mwanzoni mwa mwezi Januari.

Share this:

  • Click to share on Twitter (Opens in new window)
  • Click to share on Facebook (Opens in new window)
  • Click to share on Google+ (Opens in new window)

Related

Jumapili hii ni NIGERIA vs MOROCCO katika michuano ya AFRIKA-CHAN
KENYA: Marekani yamshutumu Odinga kwa ‘kujiapisha’

Related articles

Msanii Sam wa Ukweli ameaga…
Mazishi ya pacha Maria na…
Vladmir Putin aizuru Austria.
Jeshi la Zimamoto lakanusha madai…
TABORA: Biashara ya Magimbi yashamiri…
Serikali imetenga fedha kwa ajili…

Leave a Reply Cancel reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

On Air Now

Download CG Google App here

CLICK TO PLAY CG ONLINE TV

Advertise here

ABOUT US

CG FM RADIO is the radio station that based in Tabora – Tanzania that targets all age groups. Due to its moral observation and ethical programs, CG FM radio continues to have a lot of audience which makes us the best on western zone.

YOU ARE HOME

TWITTER

My Tweets

Menu

  • HOME
  • News
  • Listen Live
  • Advertise