Skip to content
CGFM
  • Home
  • Listen Live
  • News
  • Presenters
  • Gallery
  • Advertise
Sports

Tetesi za Soka Ulaya Jumanne 09.01.2018

  • January 9, 2018

Manchester City wanatarajiwa kutoa ofa mpya kwa mshambuliaji wa Arsenal, Alexis Sanchez, 29, na wanaamini kuwa Arsenal watamruhusu raia huyo wa Chile kuondoka mwezi huu.

Sanchez yuko tayari kurejesha kima cha pauni milioni 25 kuhakikisha kuwa amejiunga na Manchester City mwezi huu. (Sun)

Arsenal watamruhusu Sanchez kuondoka ikiwa watapokea hadi paui milioni 30 na wanataka shughuli hiyo kukamilika mapema ili kuwawezesha kumtafuta mchezaji ambaye atachukua mahala pake. (Mirror)

Taarifa zinasema kuwa Sanchez huenda akajiunga na Manchester City kwa muda wa wiki moja inayokuja. (Independent)

Arsenal wamemuorodhesha mshambuajia wa Monaco Thomas Lemar, 22, kuwa nambari moja katika kuchukua mahala pake Sanchez, baada ya kushindwa kumsaini mfaransa huyo msimu uliopita. (Mirror)

Meneja wa Monaco Leonardo Jardim hajakana kuwa kuuzwa kwa Lemar mwezi huu. (L’Equipe – in French)

Arsenal na Liverpool wana nia ya kumsaini kiungo wa kati wa Barcelona na Croatia Ivan Rakitic, 29, ambaye anataka kuondoka kufuatia kuwasili kwa Philippe Coutinho. (Diariogol – in Spanish)

Liverpool wametupilia mbalia madai kutoka Barcelona kuwa kuuzwa kwa Coutinho kwa pauni milioni 142 kulifanyika baada ya Liverpool kupunguza fedha hizo. (Times)

Kiungo wa kati wa Ufaransa Francis Coquelin, 26, ataondoka Arsenal mwezi huu, huku nao West Ham wakiwa na hamu ya kumsaini (Mirror)

alencia nao wako kwenye mazungumzo na Arsenal kuhusu Coquelin. (Cadena Ser – in Spanish)

Chelsea wamesitisha mikakati kwa kumwinda beki wa Juventus Mbrazil Alex Sandro, 26, kwa sababu klabu hiyo ya Italia inataka paunia milioni 60 kwa beki huyo. (Telegraph)

Mshambuliaji wa Tottenham na England Harry Kane, 24, anasema yuko sawa katika klabu hiyo lakini ni lazima waanze kushinda vikombe kumwezesha kubaki. (Star)

Leicester wana nia ya kumuchia mshambuliaji Kelechi Iheanacho, 21, kuondoka mwezi huu licha ya kumsani mnigeria huyo tu hivi karibu kwa pauni milioni 25. (Sun)

West Ham wanakaribia kumsaini kiungo wa kati wa England na Newcastle Jonjo Shelvey, 25, kwa pauni milioni 12. (Express)

Juventus hawatamsaini kiungo wa kati wa Lazio Sergej Milinkovic-Savic, 22, kwa sababu Paris St-Germain wanataka kutoa pauni milioni 150 kwa raia huyo wa Serbia ambaye pia amewavutia Manchester United. (Il BiancoNero – in Italian)

Newcastle watamruhusu mshambuliaji raia wa Serbia Aleksandar Mitrovic, 23, kuondoka Januari lakini wanataka kurejesha pauni milioni 18 walizotumia kumnunua miezi 18 iliyopita.

Share this:

  • Click to share on Twitter (Opens in new window)
  • Click to share on Facebook (Opens in new window)
  • Click to share on Google+ (Opens in new window)

Related

Edward Lowassa akutana na Magufuli, amsifu kwa ‘kazi nzuri’ Tanzania
Droo Kombe la FA: Liverpool uso kwa uso na West Bromwich Albion.

Related articles

Simba Yamsajili Adam Salamba.
Roman Abrahamovich ahamia Israel.
Kipa wa Liverpool atishiwa maisha.
Haji Manara, Simba na Yanga…
Serengeti Boys wa Tanzania watwaa…
Wachezaji wanajua umuhimu wa mechi…

Leave a Reply Cancel reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

On Air Now

Download CG Google App here

CLICK TO PLAY CG ONLINE TV

Advertise here

ABOUT US

CG FM RADIO is the radio station that based in Tabora – Tanzania that targets all age groups. Due to its moral observation and ethical programs, CG FM radio continues to have a lot of audience which makes us the best on western zone.

YOU ARE HOME

TWITTER

My Tweets

Menu

  • HOME
  • News
  • Listen Live
  • Advertise