Skip to content
CGFM
  • Home
  • Listen Live
  • News
  • Presenters
  • Gallery
  • Advertise

Toleo bandia la WhatsApp lapakuliwa mara milioni moja kabla…

  • November 7, 2017
Toleo bandia la WhatsApp lapakuliwa mara milioni moja.

Toleo bandia la programu ya huduma ya kutuma ujumbe ya WhatsApp lilipakuliwa zaidi ya mara milioni moja kutoka kwa programu ya Google Play Store kabla ya kuondolewa.

Programu hiyo kwa jina Update WhatsApp Messenger ilionekana kutengezwa na kampuni ilioanzisha huduma hiyo WhatsApp Inc.

Kulingana na watumiaji katika mtandao wa Reddit, huduma hiyo bandia ilikuwa na matangazo na ilikuwa ikipakua programu hiyo kwa vifaa vya watumiaji wake.

Programu hiyo sasa imeondolewa.

Waliweza kuiweka kwa kutumia jina sawa la WhatsApp.

Tofauti iliokuwepo ilikuwa vigumu sana kwa mtu wa kawaida kutambua.

Watumiaji ambao walipokea programu imara ya huduma hiyo hawakuathiriwa.

Sio mara ya kwanza kwa kampuni ya Google kulazimika kuondoa programu feki katika hifadhi yake ya Play Store.

Mwaka 2015, kampuni hiyo ililazimika kuingilia kati na kuifunga programu moja iliojidai kutathmini betri na ilikuwa ikituma ujumbe wa maandishi katika simu za wateja.

Share this:

  • Click to share on Twitter (Opens in new window)
  • Click to share on Facebook (Opens in new window)
  • Click to share on Google+ (Opens in new window)

Related

Saudia yadai Iran ilihusika katika shambulio la kombora.
WILL SMITH NA JADA PINKETT WAMCHANGIA TYRESE DOLA MILIONI 5.

Related articles

Mabaki ya ndege iliotoweka na…
Msanii Sam wa Ukweli ameaga…
Refa Mkenya aliyeteuliwa na Fifa…
Mazishi ya pacha Maria na…
Rais Madagascar ateuwa waziri mkuu…
Bodi ya usimamizi wa shule…

Leave a Reply Cancel reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

On Air Now

Download CG Google App here

CLICK TO PLAY CG ONLINE TV

Advertise here

ABOUT US

CG FM RADIO is the radio station that based in Tabora – Tanzania that targets all age groups. Due to its moral observation and ethical programs, CG FM radio continues to have a lot of audience which makes us the best on western zone.

YOU ARE HOME

TWITTER

My Tweets

Menu

  • HOME
  • News
  • Listen Live
  • Advertise