TRA mkoa wa TABORA imewataka wajasiriamali kusajili biashara zao…
Mamlaka ya Mapato nchini -TRA mkoa wa TABORA imewataka wajasiriamali kusajili biashara zao ili kuondoa usumbufu unaoweza kujitokeza wakati wa ukaguzi.
Kauli hiyo imetolewa na Afisa Kodi wa TRA mkoa wa TABORA,Bwana DAUD DOS SANTOS amesema wajasiriamali wenye biashara wanatakiwa kujisajili ili kutambua biashara zao kwa urahisi.
Amesema wajasiriamali wamekuwa wakishindwa kusajili biashara zao kutokana na kudai kuwa namba ya utambulisho wanazilipia jambo ambalo amesema wafanyabiashara wote wanapewa namba hizo bure.