Skip to content
CGFM
  • Home
  • Listen Live
  • News
  • Presenters
  • Gallery
  • Advertise
International

Trump: Mazungumzo na Korea Kaskazini ni kutupa muda.

  • October 2, 2017October 2, 2017

Rais wa Marekani Donald Trump amemuambia waziri wake wa mashauri ya nchi za nje kuwa anatupa muda wake akijaribu kufanya mazungumzo na Korea Kaskazini kuhusu mpango wake wa nyuklia.

“Jiwekee nguvu zako Rex, tutafanya kile kitahitajika kufanywa,” Bw. Trump aliandika kwenye twitter baada ya kuibuka madai kuwa Marekani ilikuwa kwenye mazungumzo na Pyongyan.

Rex alifichua hayo siku ya Jumamosi akisema kuwa Korea Kaskazini haitili maanani mazungumzo hayo.

Nchi hizo mbili zimekuwa kwenye majibizano makali miezi ya hivi karibuni.

Kombora la Majaribio la Korea Kaskazini.

Marekani inataka Korea Kaskazini kusitisha mipango yake ya silaha baada ya kufanya majaribio kadha ya makombora ya na kudai kufanya jaribo la bomu la haidrojeni ambalo linaweza kutundikwa kwa kombora la masafa marefu.

Hi sio mara ya kwanza Donald Trump amekinzana na maafisa wa vyeo vya juu kwenye utawala wake.

Mwezi Agosti alisema kuwa jeshi la Marekani lilikuwa tayari kukabiliana na Korea Kaskazini, saa chache baada ya waziri wake wa ulinzi kujaribu kutuliza misukosuko akisema kuwa jitihada za mazungumzo zilikuwa zinafanikiwa.

Matamshi yake yanakuja siku moja bada ya Bw Tillerson kufichua kuwa maafisa wa Marekani walikuwa na mawasiliano na Korea Kaskazini licha na kuwepo vita vya maneno kati ya viongozi wa nchi hizo mbili.

 

Share this:

  • Click to share on Twitter (Opens in new window)
  • Click to share on Facebook (Opens in new window)
  • Click to share on Google+ (Opens in new window)

Related

Manispaa Moshi yajitosa bomoabomoa Pasua
Wachezaji wa Soka wampinga Trump Marekani.

Related articles

Mabaki ya ndege iliotoweka na…
Refa Mkenya aliyeteuliwa na Fifa…
Rais Madagascar ateuwa waziri mkuu…
Bodi ya usimamizi wa shule…
Mchungaji auawa akiwabatiza waumini Ziwani
Guardiola alinichukulia kama adui na…

Leave a Reply Cancel reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

On Air Now

Download CG Google App here

CLICK TO PLAY CG ONLINE TV

Advertise here

ABOUT US

CG FM RADIO is the radio station that based in Tabora – Tanzania that targets all age groups. Due to its moral observation and ethical programs, CG FM radio continues to have a lot of audience which makes us the best on western zone.

YOU ARE HOME

TWITTER

My Tweets

Menu

  • HOME
  • News
  • Listen Live
  • Advertise