
Tume ya UKIMWI ZANZIBAR inakusudia kuongeza elimu kwa makundi…
Tume ya UKIMWI ZANZIBAR inakusudia kuongeza elimu kwa makundi hatarishi na vijana ili kuhakikisha maambukizi mapya ya virusi vya UKIMWI yanapunguza
Mkuu wa Uhamasishaji wa Tume ya UKIMWI ZANZIBAR ZAC bibi NURU RAMSA MBAROUK amesema kwa sasa kundi la vijana kuanzia miaka 15 hadi 24 linaonekana kuwa na maambukizi makubwa, huku utandawazi ukionekana kurahisisha vijana kupata taarifa sahihi na zisizosahihi.
Akizungumzia juu ya waajiri wanaowafukuza kazi wafanyakazi wao wanaobainika kuambukizwa virusi vya UKIMWI bibi NURU amesema ni vyema wakajitokeza ili sheria ichukue mkondo wake.