Skip to content
CGFM
  • Home
  • Listen Live
  • News
  • Presenters
  • Gallery
  • Advertise

Uchaguzi Liberia: George Weah akiri kuwasiliana na Charles Taylor.

  • October 6, 2017

Mmoja wa wagombea katika uchaguzi wa urais nchini Liberia na nyota wa soka George Weah amekiri kuwa na mawasiliano na kiongozi wa zamani wa taifa hilo Charles Taylor.

Bw Taylor anatumikia kifungo cha miaka 50 jela nchini Uingereza kwa makossa uhalifu wa kivita baada ya kuhukumiwa na mahakama maalum ya Umoja wa Mataifa.

Bw Weah amesema kuwa alipokea simu kutoka kwa mbabe huyo wa kivita, lakini akakanusha kwamba Charles Taylor ana ushawishi wa mambo nchini humo.

Wiki iliyopita, Bunge la Congress nchini Marekani liliidhinisha azimio la kushutumu juhudi zozote za mbabe huyo wa zamani wa kivita za kujaribu kuwa na ushawishi kwenye uchaguzi nchini Liberia kutoka gerezani.

George Weah ni mmoja wa wagombea 11 ambao wamejitokeza kutaka kumrithi Rais Ellen Johnson-Sirleaf ambaye anastaafu.

Makamu wa rais wa Johnson Sirleaf, Joseph Boakai, pia anawania katika uchaguzi huo utakaofanyika Jumanne tarehe 10 Oktoba.

Charles Taylor anatumikia kifungo cha miaka 50 jela Uingereza.

Kuna mwanamke mmoja pekee aliyejitokeza kuwania, MacDella Cooper, ambaye alikuwa mwanamitindo lakini kwa sasa ni mfanyakazi wa hisani.

Jewel Howard-Taylor, 54, mke wa zamani wa Charles Taylor ni mgombea mwenza wa Bw Weah.

 

 

Share this:

  • Click to share on Twitter (Opens in new window)
  • Click to share on Facebook (Opens in new window)
  • Click to share on Google+ (Opens in new window)

Related

Mauaji Las Vegas: Chama cha umiliki wa bunduki Marekani chaunga mkono mageuzi.
Diamond Platnumz atoa povu kwa wanaofuatilia maisha yake ya mahusiano.

Related articles

Mabaki ya ndege iliotoweka na…
Refa Mkenya aliyeteuliwa na Fifa…
Rais Madagascar ateuwa waziri mkuu…
Bodi ya usimamizi wa shule…
Mchungaji auawa akiwabatiza waumini Ziwani
Guardiola alinichukulia kama adui na…

Leave a Reply Cancel reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

On Air Now

Download CG Google App here

CLICK TO PLAY CG ONLINE TV

Advertise here

ABOUT US

CG FM RADIO is the radio station that based in Tabora – Tanzania that targets all age groups. Due to its moral observation and ethical programs, CG FM radio continues to have a lot of audience which makes us the best on western zone.

YOU ARE HOME

TWITTER

My Tweets

Menu

  • HOME
  • News
  • Listen Live
  • Advertise