Ugonjwa wa shinikizo la jicho wazidi kushika kasi TABORA.

Hayo yamebainishwa na Mratibu wa MACHO Mkoa wa TABORA Daktari MATIS SOSOMA akisema kuwa ugonjwa huo hauna kinga lakini mtu anapaswa kuwahi kwa wataalamu wa afya ili apatiwe matibabu mapema
Amewashauri wananchi wakiona wanasumbuliwa na maumivu ya kichwa na wamepima presha ya kawaida hawana na malaria hawana basi wasitumie dawa yoyote bali watafute mtalaam wa afya ya macho ili wapimwe presha ya macho
Daktari SOSOMA amesema sababu kubwa ya shinikizo la jicho ni pamoja na msongo wa mawazo
Amesema kuwa tatizo hilo halina kinga japo mtu anapaswa kuwahi kupatiwa matibabu huku akisema kuwa mtu atakayetibiwa hawezi kurudi katika hali yake ya kawaida bali wanazuia tatizo lisiendelee mbele libaki pale pale
Kwa upande wao,wakazi wa Halmashauri ya Manispaa ya TABORA,ALLY SELEMAN,FIKIRI GILBERT na RUTTA ELIUS wamesema watatumia njia mbali mbali kujikinga na shinikizo la jicho ikiwa ni pamoja na kuepukana na msongo wa mawazo.