
Umuhimu wa masomo ya ziada kwa Wanafunzi.
Masomo ya ziada yana umuhimu kwa wanafunzi kwa sababu wanapata muda wa kurudia walichofundishwa shuleni na kukielewa kwa undani zaidi.
Mwalimu mkuu wa shule ya msingi MIHAYO katika Halmashauri ya Manispaa ya TABORA,KASHINDE FAUSTINE amesema wazazi wanatakiwa kujitahidi ili watoto wao wahudhurie masomo ya ziada mara baada ya muda wa masomo wa kawaida ili kuwaongezea ufaulu.
Amewashauri wazazi na walezi mjini TABORA kuwa na mwamko kielimu kwa watoto ili kuwajengea uwezo wa kupenda shule na kuhudhuria masomo bila kukosa.