Urambo, TABORA: Kijana ahukumiwa jela miaka saba kwa wizi…

Kijana BARAKA SAMSONI,mkazi wa KIBAONI mkoani SINGIDA amehukumiwa na mahakama ya wilaya ya URAMBO kutumikia kifungo cha miaka SABA jela baada ya kukiri kuiba gari alilokuwa amekabidhiwa kuendesha.
Akisoma hukumu ya kesi hiyo,Hakimu Mkazi Mfawidhi wa Mahakama ya wilaya ya URAMBO,HASSAN MOMBA amesema kuwa amelazimika kutoa adhabu hiyo ili liwe fundisho kwake na kwa watu wengine wenye tabia kama hiyo.
Hakimu MOMBA amesema kuwa kitendo cha mshitakiwa kukiri kosa kunaonyesha ni jinsi gani hakuwa mwaminifu katika jamii inayomzunguka.
Awali upande wa mashitaka ukiongozwa na Mkaguzi wa Polisi PHILLERT PIMMA ulidai kuwa mtuhumiwa BARAKA SAMSONI alitenda kosa hilo tarehe 28 mwezi uliopita.
Ameongeza kuwa kuwa siku hiyo eneo la MAJENGO YA KATI mjini URAMBO mshitakiwa aliiba gari aina ya Toyota Land Cruser Pickup lenye namba za usajili T 659 CYK yenye thamani ya shilingi 75 milioni mali ya SUN ZHI,raia wa CHINA.
Mshitakiwa ambaye alikuwa ni dereva wa gari hilo baada ya wizi huo alikamatwa akiwa wilaya ya KAHAMA akiwa katika harakati za kutaka kuliuza kwa shilingi milioni TISA.