Skip to content
CGFM
  • Home
  • Listen Live
  • News
  • Presenters
  • Gallery
  • Advertise
International

Uturuki na Israel zafukuziana balozi baada ya mauaji Gaza

  • May 16, 2018

Israel imetuma malori manane ya misaada ya kiutu pamoja na dawa za matibabu katika ukingo wa Gaza, huku uhusiano wake wa kidiplomasia na Uturuki ukiwa umeingia doa baada ya wanajeshi wa Israel kuwaua Wapalestina 60.

Israel imesema Jumatano kwamba imetuma malori manane yaliyojazwa misaada ya kiutu pamoja na dawa za matibabu katika ukingo wa Gaza, baada ya wanajeshi wake kuwaua Wapalestina wapatao 60 Jumatatu iliyopita kwa kuwafyatulia risasi katika eneo la mpaka kati ya Gaza na Israel.

Kikosi cha kijeshi kwa masuala ya raia wa Palestina, Cogat, kimesema jana kwamba kimetuma tani 53 za vifaa vya matibabu huko Gaza, ikiwa ni pamoja na maji ya matibabu, bendeji na vifaa vya mazoezi ya mwili na kusema mafuta yatawasambazwa baadaye.

Wakati huo huo, Waziri Mkuu wa Israel Benjamin Netanyahu jana alijitetea kwa kusema hakujakuwa na jinsi nyingine yoyote ya kukabiliana na waandamanaji hao zaidi ya kutumia nguvu ya kijeshi. Katika mahojiano na kituo cha televisheni cha Marekani cha CBS, Netanyahu alililaumu kundi la Kipalestina la Hamas.

“Natamani yasingetokea. Lakini Hamas inayashawishi makundi ya watu kujipenyeza Israel, na dhahiri wanatangaza lengo lao la kuitokomeza Israel,” amesema benjamin Netanyahu.

Gazastreifen Proteste mit Steinschleuder (picture-alliance/NurPhoto/M. Faiz)Wapalestina wakitumi manati huku wanajeshi wa Israel wakitumi risasi za moto katika maandamano ya Gaza

Balozi zafukuzwa

Ujumbe wa kidiplomasia wa Palestina nchini Marekani umetakiwa kurudi nyumbani baada ya maandamano ya Jumatatu ya kupinga kufunguliwa ubalozi mpya wa Marekani mjini Jerusalem. Husam Zomlot amelithibitishia shirika la habari la AP kwamba ameitwa na serikali yake kurudi Palestina.

Wakati huo huo, Rais wa Uturuki Reccep Tayyip Erdogan na Waziri Mkuu wa Israel wametupiana maneno na kuwataka wanadiplomasia wao kurudi nyumbani.

Wizara ya mambo ya nje ya Uturuki imemtaka balozi wa Israel kuondoka nchini mwake baada ya kukasirishwa na kitendo cha Israel cha kutumia nguvu dhidi ya waandamanaji wa Kipalestina katika mpaka wa Gaza na uamuzi wa Marekani wa kuuhamishia ubalozi wake mjini Jerusalem. Kufuatia hatua hiyo, Israel nayo ikamtaka mkuu wa ubalozi mdogo wa Uturuki kuondoka kwa muda nchini mwake na kurudi Uturuki.

Gaza Israel Konflikt Jerusalem US Botschaft (Reuters/R. Zvulun)Binti wa Donald Trump, Ivanka Trump katika sherehe za kufungua ubalozi wa Marekani Jerisalem.

Guatemala nayo Jamatatu imefuata mfano wa Marekani na kufungua ubalozi wake mjini Jerusalem.

Juiya ya Kiarabu na Uturuki kuitisha mikutano

Vita vya maneno kupitia ukurasa wa Twitter kati ya Erdogan na Netanyahu vinatishia kuharibu makubaliano yao ya mwaka 2016 ya yaliyorejesha uhusiano wa kawaida baina yao baada ya mzozo wa miaka mingi.

Erdogan ataitisha mkutano wa kilele wa dharura Ijumaa ijayo mjini Istanbul wa Jumuiya ya Ushirikiano wa Mataifa ya Kiislamu OIC, ambao amesema utatoa kauli nzito juu ya suala hilo la mauaji ya Wapalestina yaliyofanywa na Israel.

Mataifa ya Kiarabu kwa upande wake yamelaani mauaji hayo ya Wapalestina katika maandamno ya Jumatatu huko Gaza, kama ilivyo kawaida yao ya kufanya hivyo baada ya kila vurugu zinazofanywa na Israel dhidi ya Wapalestina. Lakini kutokana na hofu ya Iran walionayo baadhi yao, viongozi wa Kiarabau wamegawanyika juu ya suala hilo. Kuna ambao wako tayari kuiunga mkono Israel kisiri siri.

Jumuiya ya Kiarabu hata hivyo nayo pia itakuwa na mkutano hapo kesho Alhamisi ulioitishwa na Saudi Arabia kujadili mgogoro wa Israel na Palestina.

Mwandishi: Yusra Buwayhid/ap/afp

Mhariri: Caro Robi

CHANZO: DW Kiswahili.

Share this:

  • Click to share on Twitter (Opens in new window)
  • Click to share on Facebook (Opens in new window)
  • Click to share on Google+ (Opens in new window)

Related

Kenya yaidhinisha sheria sheria ya kueneza habari feki.
Wahamiaji Haramu 120 wakamatwa Tabora.

Related articles

Mabaki ya ndege iliotoweka na…
Refa Mkenya aliyeteuliwa na Fifa…
Rais Madagascar ateuwa waziri mkuu…
Bodi ya usimamizi wa shule…
Mchungaji auawa akiwabatiza waumini Ziwani
Volkano yasabisha vifo vya watu…

Leave a Reply Cancel reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

On Air Now

Download CG Google App here

CLICK TO PLAY CG ONLINE TV

Advertise here

ABOUT US

CG FM RADIO is the radio station that based in Tabora – Tanzania that targets all age groups. Due to its moral observation and ethical programs, CG FM radio continues to have a lot of audience which makes us the best on western zone.

YOU ARE HOME

TWITTER

My Tweets

Menu

  • HOME
  • News
  • Listen Live
  • Advertise