Uwepo wa mabaraza ya wazee visiwani ZANZIBAR umesaidia wazee…
Uwepo wa mabaraza ya wazee visiwani ZANZIBAR umesaidia wazee kwa kiasi kikubwa kutokata tamaa ya maisha na kuishi katika maisha mazuri kama watu wengine
Katibu wa Jumuiya ya wastaafu na wazee ZANZIBAR,SALAMA AHMED amebainisha hayo wakati akizungumza katika kikao cha kamati ya Jumuiya hiyo na bodi ya wajumbe wa shirika la kuhudumia wazee duniani kilichofanyika katika ukumbi wa Mfuko wa Hifadhi ya Jamii ZANZIBAR- ZSSF KILIMANI mjini UNGUJA
Amesema shirika la kuhudumia wazee duniani limesaidia kuundwa kwa mabaraza ya wazee na kusaidia wazee kutumia mabaraza hayo katika kutatua matatizo yao.
Naye Mfanyakazi wa Wizara ya afya OMAR MAALIM OMAR amesema shirika la kuhudumia wazee limefarijika kuona wazee wa ZANZIBAR wanapata mafao ya pensheni bila ya ubaguzi.