
Uzalishaji wa zao la Nazi washuka Zanzibar.
Uzalishaji wa zao la nazi ZANZIBAR ni mdogo kutokana na ujenzi wa makazi ya watu katika maeneo yaliyotengwa kwa ajili ya kilimo cha minazi.
Katibu Mkuu wa Wizara ya Biashara,Viwanda na Masoko,JUMA ALI JUMA amesema uvunaji wa nazi ZANZIBAR ni mdogo licha ya kuwepo kwa mahitaji makubwa ya matumizi kwa wananchi.
Katibu Mkuu huyo amefafanua kuwa upungufu wa zao la nazi huko ZANZIBAR ulianza mwaka 1970 na hadi sasa mahitaji ya nazi bado hayajafikiwa.
Ameongeza kwamba upo umuhimu wa kuzalisha nazi ili kupatikana malighafi kwa matumizi ya ndani ya nyumbani na kwenye viwanda vya kutengenezea sabuni nchini.