Vilabu vinavyoshiriki ligi ya mkoa wa TABORA kutoka wilaya…
Vilabu vinavyoshiriki ligi ya mkoa wa TABORA kutoka wilaya ya UYUI vimehakikishiwa kupewa ushirikiano kutoka katika wilaya hiyo.
Akizungumza na CG FM,Afisa Utamaduni wilaya ya UYUI,DAUDI DANGUCHE amesema ameweka mkakati wa kuvisaidia vilabu hivyo.
Wilaya ya UYUI itawakilishwa na vilabu vya NSAGUZI FC,TURA FC na IKONGOLO FC na ligi ya mkoa wa TABORA itaanza pindi vilabu vyote vikilipa ada ya ushiriki.