Skip to content
CGFM
  • Home
  • Listen Live
  • News
  • Presenters
  • Gallery
  • Advertise
International

Volkano yasabisha vifo vya watu 65 hadi sasa.

  • June 5, 2018

Mlipuko wa Volcano ulioikumba Guatemala hadi sasa imesababisha vifo vya watu 65.Vikosi vya uokoaji vimebaini miili Zaidi kutoka katika vijiji vilivyopo chini ya mwinuko wa eneo la Fuego lililokumbwa na Volcano hiyo na bado idadi kubwa ya watu hawajulikani walipo hadi sasa.

Taarifa zinasema kuwa zaidi ya watu 4,000 wameokolewa kutoka eneo la kusini magharibi mwa Guatemala,umbali wa kilomita 35 ambalo limeathirika na moshi wa Volcano hiyo pamoja uji wa lava.

Watu milioni moja nukta saba sawa na zaidi ya asilimia 10 ya watu wote wapo katika hatari kubwa ya kukumbwa na madhara ya Volcano hiyo.

Luiz Meléndez ni mratibu wa majanga wa eneo la Escuintla.Anasema kuwa maandalizi yanaendelea kuhakikisha kuna maeneo ya kutosha kuwahifadhi wahanga wa tukio hilo.

“Tathimini kwaajili ya kuandaa mazingira ya kuwahifadhi watu inaendelea,ambayo inazingatia pia masuala ya usalama na mahitaji muhimu ya kuwa nayo,ili wananchi wasipate shida pale watakapopelekwa katika eneo la hifadhi.”Luis Melendez.

Vikosi vya wanajeshi pia wanasaidi kuzima moto na kusaka watu ambao hadi sasa hawajulikani walipo

Jorge Luis Altuve ambaye ni mmoja wa brigade ya uokoaji iliyopo milimani,ameiambia BBC kwamba wameanza kushuka kutoka maeneo hayo ya mlimani kwani kumeanza kumekumbwa na giza na hivyo kutishia usalama wao pia.Serikali ya Guatemala imesema kuwa majivu ya volkano kutoka mlima mmoja unaoendelea kulipuka, yamesababisha vifo vya watu saba na kuwajeruhi wengine ishirini.

Shirika la kukabiliana na majanga nchini Guatemala limesema kuwa mlima Fuego ulilipuka siku ya jumapili, huku majivu hayo yakirushwa hadi kijiji cha El Rodeo na kusababisha uharibifu mkubwa wa makaazi ya watu.

Baadhi yao waliteketea ndani ya nyumba hizo.

Rais wa taifa hilo Jimmy Morales amesema vikosi vya uokoaji vimeanza kazi na tahadhali imetolewa.

Hata hivyo ya watu hao waliokufa kati yao watatu ni watoto.

Mlima Fuego ukifuka moshi baada ya Volkano kulipukaMoshi ukifuka baada ya Volkano kulipuka

Mlipuko wa Volcano hii unatajwa kuwa Zaidi tangu ule uliotokea mwaka 1974.

Serikali ya Guatemala inasema kuwa takribani watu milioni moja wameathirika kutokana na Volcano hiyo.

Hata hivyo ushauri umetolewa kwa raia kuvaa vifaa vya kuzuia pua zao kutokana na moshi na majivu yanayoendelea kurushwa kutokana na Volcano hiyo.

Watoto kadhaa ni miongoni mwa waliothibitishwa kufariki.

Mitaa imejaa jivu linalotokana na volkanoMitaa imejaa jivu linalotokana na volkano

Video zilizochapishwa na vyombo vya habari nchini zinaonyesha miili ikiwa imetapakaa juu ya lava na maafisa wa uokozi wakiwahuhudmia watu waliofunikwa kwa jivu.

Mwanamke mmoja ameeleza kwamba lava ilimwagika katika mashamba ya mahindi na andhani kwamba huedna watu zaidi wamefariki.

Jumla ya watu milioni 1.7 wameathirika na mlipuko huo wa volkano, serikali ya Guatemala inasema.

Share this:

  • Click to share on Twitter (Opens in new window)
  • Click to share on Facebook (Opens in new window)
  • Click to share on Google+ (Opens in new window)

Related

Burundi kuitambulisha katiba mpya siku ya Alhamis
Guardiola alinichukulia kama adui na alinonea wivu, Yaya Toure.

Related articles

Mabaki ya ndege iliotoweka na…
Refa Mkenya aliyeteuliwa na Fifa…
Rais Madagascar ateuwa waziri mkuu…
Bodi ya usimamizi wa shule…
Mchungaji auawa akiwabatiza waumini Ziwani
Burundi kuitambulisha katiba mpya siku…

Leave a Reply Cancel reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

On Air Now

Download CG Google App here

CLICK TO PLAY CG ONLINE TV

Advertise here

ABOUT US

CG FM RADIO is the radio station that based in Tabora – Tanzania that targets all age groups. Due to its moral observation and ethical programs, CG FM radio continues to have a lot of audience which makes us the best on western zone.

YOU ARE HOME

TWITTER

My Tweets

Menu

  • HOME
  • News
  • Listen Live
  • Advertise