Vyandarua 28,200 vimetolewa kwa wanafunzi wa shule za msingi…

Zaidi ya vyandarua 28,200 vimetolewa kwa wanafunzi wa shule za msingi 79 katika Halmashauri ya Manispaa ya TABORA ili kukabiliana na ugonjwa wa malaria.
Mratibu wa afya mashuleni wa Manispaa ya TABORA,FRANCIS WAWA amesema vyandarua hivyo vilianza kusambazwa mwezi uliopita.
Jamii imeaswa kutumia vizuri vyandarua hivyo kwa sababu lengo la serikali ni kupunguza athari za ugonjwa wa malaria.