
Wafanya Biashara soko la Kachoma watakiwa kulipia kodi za…
Halmashauri ya manispaa ya TABORA imewataka wafanyabiashara katika soko la KACHOMA kulipia kodi za pango la vibanda waendelee na biashara katika maeneo yao.
Mkurugenzi wa manispaa ya TABORA,BOSCO NDUNGURU amesema kodi ya pango ni shilingi elfu hamsini kwa mwezi lakini wafanyabiashara katika soko la KACHOMA hawajalipa na kulazimika kuwafungia vibanda vyao.
Amesema wafanyabiashara katika masoko mengine wamekwishalipa lakini wafanyabiashara wa soko la kachoma wamegoma na kwamba halmashauri inasimamia sheria mpaka fedha hizo zitakapolipwa.
Amesema kama wafanyabiashara hao hawatalipa kodi za pango,vibanda hivyo vitatolewa kwa wafanyabishara wengine.