
Wajawazito washauriwa kuhudhuria klinik mara kwa mara.
Wanawake wajawazito wameshauriwa kuhudhuria kliniki mara kwa mara ili kama kuna tatizo tumboni liweze kupatiwa ufumbuzi mapema na kujiepusha kujifungua viumbe visivyokamilika.
Akizungumzia tukio la mwanamke mmoja mkazi wa kijiji cha MSWA,kata ya ISIKIZYA wilayani UYUI kujifungua yai siku chache zilizopita,Kaimu Mganga Mfawidhi wa zahanati ya ISIKIZYA,VICENT MGAYA amesema tukio hilo siyo la kawaida na kama mwanamke huyo angehudhuria kliniki tatizo hilo lingegundulika mapema.
Kwa upande wake,mwanamke aliyejifungua Yai,MAGRETH SHIJA amekiri kutohudhuria kliniki na kwamba alikuwa na ujauzito wa miezi minane ndipo alipopata uchungu wa uzazi na kujifungua yai.