
Wakurugenzi watakiwa kuwapa 4% ya fedha za halmashauri kama…
Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto UMMY MWALIMU ametoa miezi mitatu kwa wakurugenzi wote nchini kuhakikisha wanatenga asilimia 4 za fedha za halmashauri kwaajili ya kuwapa wanawake mikopo ili waweze kujikwamua kiuchumi.
Amesema kuwa serikali haitasita kuwawajibisha wakurugenzi watakaokiuka maelekezo ya serikali yanayolenga kutekeleza ahadi za Mheshimiwa Rais kwa wananchi ili kuwawezesha wanawake wa mijini na vijijini kiuchumi na hatimaye kujiongezea kipato na kuwezesha uchumi wa viwanda.
Amesema kama mkurugenzi anashindwa kutenga fedha kwaajili ya kuwapatia wanawake mikopo hatawaelewa, na ifikapo mpaka tarehe 30 June 2018 wakurugenzi wote ambao hawajatenga fedha na kuzitoa kwaajili ya wanawake majina yao yatapelekwa kwa rais.
Halikadhalika Mh. Ummy amepiga marufuku suala la kutoa fedha ndogo kwa kikundi kikubwa cha kinamama huku akitolea mfano kikundi cha watu sita kupewa 300,000 kuwa haitawasaidia kinamama hao katika juhudi za kujikwamua kiuchumi na kuongeza kuwa ni heri fedha hizo zikabaki kwa mkurugenzi ili ifanye shughuli nyingine lakini sio kuwakwamua kinamama.
Ameyasema hayo katika maadhimisho ya kilele cha Siku ya Wanawake Duniani jana yaliyofanyika katika Halmashauri ya Manispaa ya Sumbawanga mkoani Rukwa.