Walimu,wanafunzi na kamati za shule wilayani IGUNGA wametakiwa kushirikiana…

Walimu,wanafunzi na kamati za shule wilayani IGUNGA wametakiwa kushirikiana katika kutunza miti inayopandwa shuleni.
Walimu,wanafunzi na kamati za shule wilayani IGUNGA wametakiwa kushirikiana katika kutunza miti inayopandwa shuleni.
Kauli hiyo imetolewa na Afisa Misitu wa Halmashauri ya wilaya ya IGUNGA,DHAHIR KITIA wakati wa ziara ya kujifunza jinsi ya upandaji miti kwa kuzingatia sheria.
Amesema kuwa mradi wa IGUNGA ECO VILLAGE umewashirika wazazi,wanafunzi na walimu na kufanikiwa kupanda miti ambayo mpaka sasa inaendelea kustawi vizuri.
Kwa upande wake,Afisa Msaidizi wa Masuala ya Mazingira kutoka katika Mradi wa IGUNGA ECO VILLAGE,JOSEPH MAFURU amesema wameweza kuitunza miti hiyo katika kijiji cha MWANG’HARANGA.
Baadhi ya walimu wa Mazingira katika ya shule za msingi ya Mtakatifu LEO,MWENGE na HANI HANI, Mwalimu TRASIUS SIMBA,FADHILI KITANGE na SCOLASTINA MATABO wamesema fursa ya kutembelea miradi ya IGUNGA ECO VILLAGE imewawezesha kutumia mbinu bora za upandaji miti.
Mradi wa IGUNGA ECO VILLAGE umetoa fursa ya kujifunza kwa vitendo kwa wanafunzi 26 wa shule za sekondari,msingi na walimu 13 wa mazingira wilayani IGUNGA.