
Wanafunzi wa darasa la 2-5 hawajui kusoma, kuhesabu na…
Jumla ya wanafunzi 46 wa darasa la pili hadi la tano katika shule ya msingi GOWEKO wilayani UYUI hawajui kusoma,kuandika na kuhesabu.
Mwalimu mkuu msaidizi wa shule ya msingi GOWEKO,NAZIEL ANTHONY amesema sababu ya kuwa na idadi kubwa ya wanafunzi wasiojua kusoma,kuandika na kuhesabu shuleni hapo ni utoro wa rejareja na idadi kubwa ya wanafunzi katika darasa moja.
Mwalimu mkuu wa shule ya msingi GOWEKO RAMADHANI JUMA amesema idadi ya wanafunzi wasiyojua kusoma, kuandika na kuhesabu ni ndogo ikilinganishwa na wanafunzi wa aina hiyo mwaka jana.
Mwalimu mkuu wa masaidizi NAZIEL ametaja mikakati ya kupuguza wanafunzi wasojua kusoma, kuhesabu na kuandika ikiwa ni pamoja na kushirikiana na wazazi kuwahimiza wanafunzi sugu kwa utoro kuhudhuria masomo.
Ameongeza kuwa mkakati mwingine alianza tangu mwezi januari ni kuwafundisha muda wa ziada kwanzia satisa alasiri hadi sakumi.
Pia idadi hiyo kubwa ya wanafunzi wasojua kusoma kuhesabu na kuandika ni miongoni mwa mambo yaliyosababisha shule hiyo kufanya vibaya katika matokeo ya darasa la saba ambapo kati ya shule 46 za wilaya ya UYUI GOWEKO ilishika nafasi ya 45.