Wananchi mkoani TABORA wametakiwa kutunza Misitu ili kupata mvua…

Wananchi mkoani TABORA wametakiwa kutunza Misitu ili kupata mvua za kutosha na kuuepusha Mkoa kuingia katika janga na kukosa chakula.
Wito huo umetolewa na Afisa Misitu wa Wilaya ya IGUNGA Bwana JAHULULA EDWARD akisema kuwa wananchi walio wengi hawana uelewa kwamba uharibifu wa misitu ni moja ya sababu ya kukosekana kwa mvua ambayo itasababisha kukosekana kwa chakula.
Ameongeza kuwa ni vyema wakulima wakabadilika sasa na kuanza kulima mazao ya chakula na biashara ili kujikinga na baa la njaa na kuachana na tabia ya kuchagua vyakula
Naye Bwana AMONI MOSHI amabye ni Afisa Maliasili wa Wilaya ya IGUNGA amesema kuwa kufuatia kauli ya serikali kwamba hawatatoa chakula hivyo ni vyema wananchi wakatumia njia bora za kilimo na kutunza vyakula walivyonavyo.
Nao baadhi ya wananchi katika kijiji cha MWABAKIMA Wilayani IGUNGA Bi RACHEL TUPA, JILEMBA MAGIRI na Bi ASHURA JUMA wamesema si vyema serikali kuwanyima chakula kwa sababu hali ya mvua msimu uliopita haikuwa nzuri na kusababisha uhaba wa chakula
Kila ifikapo Oktoba 16 Dunia huadhimisha siku ya chakula dunia na kauli mbiu ya mwaka huu ni kubadili mwelekeo wa wahamiaji.