Wananchi wa mkoa wa TABORA wametakiwa kutunza mazingira na…

Wananchi wa mkoa wa TABORA wametakiwa kutunza mazingira na kutumia njia mbadala za kukabiliana na mabadiliko ya tabia nchi.

Wito huo umetolewa na mkuu wa mkoa wa TABORA,Bwana AGGREY MWANRY wakati akitembelea miradi ya kijiji cha ECO kilichoko kata ya MBUTU wilayani IGUNGA.
Akitoa maelezo kuhusu ujenzi wa tenki la maji la kijiji cha MWABAKIMA katika kata MBUTU,Meneja Mradi,Bi STELLAH THOMAS amesema mafundi wenye ujuzi walijenga tenki hilo na kusaidia shughuli za zahanati katika kijiji hicho.