Wananchi wa wilaya ya NZEGA mkoani TABORA kujiandaa kwa…

Mkuu wa wilaya ya NZEGA mkoani TABORA,GODFREY NGUPULA amewataka wananchi wa kijiji cha KISHIRI katika kata ya MWAMALA wilayani humo wanaonufaika na Mpango wa Mfuko wa Maendeleo ya Jamii nchini –TASAF wa kunusuru kaya maskini awamu ya tatu kuhakikisha wanajishughulisha kwa kilimo kwa kuzitumia mvua za kwanza zitakazoanza kunyesha mwishoni mwa mwezi huu.
Ametoa wito huo wakati akizungumza na wakazi wananchi juu ya kujiendeleza kiuchumi kupitia mpango wa TASAF awamu ya tatu.
NGUPULA amesema ili wanufaika hao waweze kujikwamua kiuchumi wanatakiwa kujikita katika shughuli za kilimo kwa kulima mazao yatakayoendana na hali ya hewa pamoja na kupanda mapema mwanzoni mwa msimu wa mvua.
Amesema iwapo walengwa hao watalima mazao yao mapema itawasaidia kuvuna kwa wingi kwani yatakua yameiva kutokana na mvua zitakazokua zimenyesha mwanzoni mwa msimu wa kilimo.
Naye Kaimu Afisa wa TASAF wilayani NZEGA,ANTONY SEBASTIAN amesema zoezi la kuzinsuru kaya maskini limekua likiendelea vizuri na mabadiliko mbalimbali yameonekana kwa walengwa na kwamba wengi wao wamekua wakibuni miradi endelevu.