
Wananchi wahimizwa kushiriki kikamilifu maadhimisho ya Mei Mosi.
Wananchi wa mkoa wa TABORA kutakiwa kushirikia kikamilifu katika maadhimisho ya Siku ya Wafanyakazi Duniani
Wananchi wa mkoa wa TABORA wametakiwa kuonesha umoja na mshikamano kwa kushiriki kikamilifu katika maadhimisho ya ya Siku ya Wafanyakazi Duniani-MEI MOSI.
Wito huo umetolewa na Mratibu wa sherehe za Mei Mosi mwaka huu,GRATION MBEYUNGE ambaye pia ni Katibu wa chama cha wafanyakazi wa Viwanda,Biashara,Taasisi za Fedha,Huduma na Ushauri TUICO mkoa wa TABORA wakati akizungumzia maandalizi ya sherehe hizi zitakazofanyika Kimkoa wilayani NZEGA.
Awali akizungumzia historia ya maadhimisho ya sherehe za Mei MOSI,MBEYUNGE amesema TANZANIA inaungana na nchi nyingine Duniani kuweka kumbukumbu muhimu ya wafanyakazi.
Akizungumza na CG FM,Katibu wa chama cha wafanyakazi wa Taasisi za Elimu ya Juu, Sayansi,Teknolojia,Habari na Utafiti nchini- RAAWU na Mratibu wa Shirikisho la Vyama huru vya Wafanyakazi -TUCTA mkoa wa TABORA,ALEX BYANGWAMU amewataka wananchi wa wilaya ya NZEGA kuitumia fursa hii kikamilifu kujiimarisha kiuchumi.
Nao Baadhi ya wananchi wa wilaya ya NZEGA wamefurahishwa na hatua ya maadhimisho YA Siku ya Wafanyakazi Duniani kufanyika wilayani humo kama wanavyobainisha.
Maadhimisho ya sherehe za Siku ya Wafanyakazi Duniani mwaka huu yanafanyika kitaifa mkoani IRINGA yakiongozwa na kauli mbiu –Kuunganishwa kwa Mifuko ya Hifadhi ya Jamii kulenga kuboresha Mafao ya Wafanyakazi na mgeni rasmi atakuwa ni Rais Daktari JOHN POMBE MAGUFULI.