Wananchi wameeleza kuwa viwango vya rushwa vimepungua nchini.
Wananchi wameeleza kuwa viwango vya rushwa vimepungua nchini.
Utafiti wa Taasisi ya TWAWEZA inasema kuwa mwaka huu ni asilimia 85 ya wananchi walioripoti vitendo vya rushwa ikilinganishwa na mwaka 2014 ambapo asilimia 78 walisema viwango vya rushwa vilikuwa vikubwa kuliko miaka 10 iliyopita.
Wananchi pia wanaripoti kuwa uzoefu wao wa kuombwa rushwa umepungua katika sekta zote mwaka 2017 ukilinganisha na mwaka 2014.
Wananchi wanaripoti kuombwa rushwa na polisi kwa asilimia 39 wakati mwaka 2014 asilimia ilikuwa 60,Idara ya maji asilimia 18 tofauti na asilimia 32 ya mwaka 2014, idara ya ardhi mwaka huu waliombwa rushwa kwa asilimia 18 wakati mwaka 2014 ilikuwa asilimia 32.
Idara nyingine zilizotajwa na wananchi kuombwa rushwa ni Mamlaka ya Mapato TANZANIA-TRA,Afya na Asasi za kiserikali.
Sekta pekee ambayo rushwa iliripotiwa kubaki vilevile ni sekta ya ajira ambapo asilimia 34 ya wananchi waliripoti kuombwa rushwa mwaka 2014 huku asilimia 36 wakiombwa rushwa mwaka 2017.