Wananchi wanaoishi karibu na maeneo ya dampo ya KARIAKOO…

Wananchi wanaoishi karibu na maeneo ya dampo ya KARIAKOO katika halmashauri ya Manispaa ya TABORA wametakiwa kuacha kuchoma moto dampo hilo kwa lengo la kuokota vyuma au malighafi mbalimbali ili kuepuka madhara wanayoweza kupata.
Wito huo umetolewa na Afisa Afya Mkuu wa Manispaa ya TABORA,PASCHAL MATAGI akisema halmashauri imejipanga kujenga dampo la kisasa baada ya kutengewa maeneo mawili ya ujenzi wa dampo hilo.
Amewataka wananchi kuwa makini kwa sababu moshi wanaochoma unaanza kuwaathiri wao wenyewe sambamba na watoto kutokana na hewa wanayovuta.