
Wananchi washauriwa kwenda kwenye vituo vya msaada wa kisheria…
Wananchi wa Halmashauri ya Manispaa ya TABORA wamehimizwa kwenda kwenye vituo vya msaada wa kisheria na haki za binadamu ili kupata elimu itakayowasaidia kukabiliana na vitendo mbalimbali vyaunyanyasaji wa kijinsia.
Mwanasheria kutoka kituo cha Msaada wa Kisheria na Haki za Binadamu-PARAREGAL- mkoa wa TABORA,HOSEA KAPONYA amesema kituo hicho cha Msaada wa Kisheria na Haki za Binadamu kwa mwaka 2017 kilifanikiwa kuifikisha elimu kwa jamii kwa asilimia themanini.
Amesema mwaka jana,wakazi wa Manispaa ya TABORA mia tano na thelathini na mmoja walikwenda katika kituo hicho kwa ajili ya kupata msaada wa kisheria na walitatuliwa kero zao na kupatiwa ufumbuzi wa kudumu.
GEODENS JOHN ni mmoja kati ya mwananchi aliyewahi kwenda kwenye kituo hicho na kutatuliwa changamoto iliyokuwa inamkabili amesema wasaidizi wa kisheria wana umuhimu sana katika jamii kwa sababu wanaisaidia jamii kujua haki zao za msingi.
Mwaka 2017 kituo cha msaada wa kisheria na haki za binadamu mkoani TABORA hicho kimefanikiwa kupunguza kiwango cha unyanyasaji wa kijinsia kwa watoto na wanawake katika Manispaa ya TABORA kwa kutoa ushauri na elimu ya msaada wa kisheria.