Skip to content
CGFM
  • Home
  • Listen Live
  • News
  • Presenters
  • Gallery
  • Advertise

Wanasayansi watengeneza kinga mpya ya mwili inayoweza kushambulia 99%…

  • September 22, 2017
Majaribio ya kinga kinga hiyo ya mwili kwa binadamu yataanza kufanyika mwaka 2018 kuangalia kama dawa hiyo inaweza kuzuwia ama kutibu maambukiziya HIV

Wanasayansi wamekuwa wakitengeneza chembe chembe za kinga ya mwili zinazoweza kushambulia asilimia 99% ya virusi vya HIV vinavyosababisha ukimwi na hivyo kuzuwia maambukizi kuendelea.

Chembe chembe hiyo ya kinga imetengenezwa kwa ajili ya kushambulia sehemu tatu muhimu za virusi na hivyo kuvifanya virusi hivyo kushindwa kuhimili mashambulizi yake.

Kazi ya utengenezaji chembe chembe hizo za kinga ya mwili imetokana na ushirikiano baina ya Taasisi ya Marekani ya Afya na kampuni maduka ya dawa ya Sanofi.

Shirika la kimataifa la kukabiliana na ukimwi -International Aids Society linasema kuwa huu ni “ugunduzi wa kihistoria “.

Majaribio ya kinga kinga hiyo ya mwili kwa binadamu yataanza kufanyika mwaka 2018 kuangalia kama dawa hiyo inaweza kuzuwia ama kutibu maambukiziya HIV

Miili yetu huhangaika kupigana na virusi vya HIV kwasababu virusi hivyo vina uwezo mkubwa wa kujibadilisha katika hali nyingine pamoja na muonekano wake.

Aina kadhaa za virusi vya HIV – katika mgonjwa mmoja zinaweza kufananishwa na zile za mafua wakati wa msimu wa baridi.

Kwa hiyo mfumo wa kinga ya mwili najipata katika vita dhidi ya magonjwa kadhaa nyemelezi yanayosababishwa na HIV.

Lakini baada ya miaka kadhaa ya maambukizi, wagonjwa wachache hujenga silaha kali ya mwili ambapo ” Mwili hupunguza uharibifu wa kinga ya mwili ” kwa kushambulia kwa kiasi kikubwa maambukizi ya HIV.

Watafiti wamekuwa wakijaribu kutumia uwezo wa mwili wenyewe wa kupunguza uharibifu wa kinga ya mwili kama njia ya kutibu HIV, ama kuzuwia maambukizi hayo mapema.

Share this:

  • Click to share on Twitter (Opens in new window)
  • Click to share on Facebook (Opens in new window)
  • Click to share on Google+ (Opens in new window)

Related

Leo ikiwa ni mwaka mpya wa kiislamu,waislamu mkoani TABORA wametakiwa kujitathmini na kujikita katika uchamungu.
Upatikanaji wa maji katika mji wa TABORA umepungua kutoka mita za ujazo milioni 17 hadi milioni 10 kwa sasa.

Related articles

Mabaki ya ndege iliotoweka na…
Refa Mkenya aliyeteuliwa na Fifa…
Rais Madagascar ateuwa waziri mkuu…
Bodi ya usimamizi wa shule…
Mchungaji auawa akiwabatiza waumini Ziwani
Volkano yasabisha vifo vya watu…

Leave a Reply Cancel reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

On Air Now

Download CG Google App here

CLICK TO PLAY CG ONLINE TV

Advertise here

ABOUT US

CG FM RADIO is the radio station that based in Tabora – Tanzania that targets all age groups. Due to its moral observation and ethical programs, CG FM radio continues to have a lot of audience which makes us the best on western zone.

YOU ARE HOME

TWITTER

My Tweets

Menu

  • HOME
  • News
  • Listen Live
  • Advertise