Skip to content
CGFM
  • Home
  • Listen Live
  • News
  • Presenters
  • Gallery
  • Advertise
International

Wanawake DRC wanapigania haki zao kumiliki ardhi

  • March 9, 2018

Wanawake wanaoishi vijijini huko Jamhumuri ya Kidemokrasi ya Kongo, hawana haki ya urithi wa mali pamoja na ardhi iliyoachwa na wazazi wao au waume zao.

Na hii inatokana na mila na desturi zao zinazomtambua mwanaume kama mrithi pekee wa Ardhi.

Wanaharakati wa haki za wanawake nchini humo wako katika jitihada za kuwaelimisha jamii kuhusiana na madhara ya mila hizo.

Wanaweke wanaoishi vijijini katika jimbo la Congo central hawana haki ya urithi mali au ardhi ya wazazi au waume zao.

Mila ya jimbo hilo inapinga kabisa kumpa mke urathi.

Image caption Licha ya kwamba marehemu babake na mume wake walimiliki hekta nyingi za ardhi, Anny mambweni haruhusiwi kurithi mali hiyo.

Katika shamba la mama Anny mambweni, anajaribu kuondosha majani shambani .

Mjane huyu wa miaka 48 ametupika sana, ana watoto watano.

Huku jasho likimtiririka usoni anaonekana akishughulika katika shamba lake – ardhi alioikopesha.

Licha ya kwamba marehemu babake na mume wake walimiliki hekta nyingi za ardhi, mila na desturi haimrusu kurithi mali hiyo.

Anny anasema ana haki kama ndugu zake wa kiume kurithi mali hiyo ilioachwana marehemu babake, lakini nduguzangu wakiume walikataa kumpa hata kipande cha ardhi.

‘Eti mwanamke hana haki ya kupewa urithi. Tizama hapa, nimelazimika kuilipa ardhi hii ninayolima ilhali babangu aliacha pori kubwa na ardhi.

Tizama, na teswa kabisa mimi na watoto wangu, nadhani mila kama hio ni mila ambayo inastahili kufutwa kwani haiku ambatana na sheria’ anasema Anny.

Mkuu wa kijiji hicho bwana Zuanikibeni Bungalo anasema ni vigumu kwa mila kubadilishwa.

‘Mwana mke atabaki kuwa mwanamke tu, unajuwa mwanamume ndio ataendesha kizazi na yeye tu ndiye anayestahili kupewa urithi wa jamaa, hatuwezi kukiuka mila yetu ata siku moja’ amesema Bungalo.

Lakini sauti zimeanza kupazwa sasa ili kuukataa utamaduni huu.

Alphonsine Ponga ni mwanaharakati wa kutetea haki za akina mama katika kijiji cha Mbaza Ngungu.

Yeye pia alikuwa mwathirika wa utamaduni huu.

“Hio ni haki yetu, ni lazima tusimame, na kama umeona tatizo hilo nenda ukashtaki mahakamani

Alphonsine Ponga, Mwanaharakati wa wanawake DRC”

‘Wanawake wengi hapa wanaogopa sana, hawapendi tufuatilie swali hilo, hilo ndio tatizo.

Nimewaeleza hio ni haki yetu, ni lazima tusimame, na kama umeona tatizo hilo nenda ukashtaki mahakamani’.

Ponga ameeleza kwamba sheria ya Congo haina ubaguzi katika suala la urithi. Lakini katika hali kawaida , ni mila ndo imeendelea kukithiri zaidi ya sharia ya nchi hasa katika maeneo ya vijijini.

Share this:

  • Click to share on Twitter (Opens in new window)
  • Click to share on Facebook (Opens in new window)
  • Click to share on Google+ (Opens in new window)

Related

TABORA: Jamii na wadau mbalimbali wahimizwa kuwaunga mkono watu wenye ulemavu
TABORA:Mradi wa ujenzi wa vyumba 3 vya madarasa wakaribia kukamilika

Related articles

Mabaki ya ndege iliotoweka na…
Refa Mkenya aliyeteuliwa na Fifa…
Rais Madagascar ateuwa waziri mkuu…
Bodi ya usimamizi wa shule…
Mchungaji auawa akiwabatiza waumini Ziwani
Volkano yasabisha vifo vya watu…

Leave a Reply Cancel reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

On Air Now

Download CG Google App here

CLICK TO PLAY CG ONLINE TV

Advertise here

ABOUT US

CG FM RADIO is the radio station that based in Tabora – Tanzania that targets all age groups. Due to its moral observation and ethical programs, CG FM radio continues to have a lot of audience which makes us the best on western zone.

YOU ARE HOME

TWITTER

My Tweets

Menu

  • HOME
  • News
  • Listen Live
  • Advertise