Wanawake wajawazito washauriwa kujua maendeleo ya ujauzito kutumia mashine…

Wanawake wajawazito mkoani TABORA wameshauriwa kupima angalau mara mbili kwa kutumia mashine ya ULTRASOUND ili waweze kujua maendeleo ya mtoto awapo tumboni.
Wito huo umetolewa na Daktari DEUSI KITAPONDYA wa Chuo Kikuu cha Sayansi MUHIMBILI ambapo amesema kupima kwa kutumia mashine ya ULTRASOUND kuna umuhimu mkubwa hasa kwa wanawake wajawazito na watu wanaopata ajali.

Kwa upande wao baadhi ya wananchi katika halmahsauri ya Manispaa ya TABORA,Bwana HAMISI WASAGA,JUMANNE HASSANI na ANGELINA ELIAS wamesema mashine ya ULTRASOUND inarahisisha huduma hospitalini,lakini wakalamikia madhara yatokanayo na mashine hizo.
Akijibu malalamiko hayo Daktari KITAPONYA amesema mashine ya ULTRASOND haina madhara yoyote na kusema hiyo ni imani potofu zilizopo kwenye jamii.
Wananchi wameshauriwa kuondokana na dhana potofu juu ya matumizi ya mashine ya ULTRASOUND na badala yake kupima kwa kutumia mashine hiyo kwa sababu haina madhara yeyote