Skip to content
CGFM
  • Home
  • Listen Live
  • News
  • Presenters
  • Gallery
  • Advertise

Wasiwasi kuhusu ‘wanyonyaji damu’ Malawi

  • October 11, 2017
Mauaji hayo yamemsikitisha sana Rais wa Malawi Arthur Peter Mutharika.

Watu watano wameuawa kusini mwa Malawi baada ya kudaiwa kuwa na sifa na tabia za watu ambao huwanyonya wengine damu.

Umoja wa Mataifa umewaondoa wafanyakazi wake katika wilaya mbili kusini mwa nchi hiyo huku wasiwasi ukiendelea kuenea.

Taarifa zinasema marehemu waliuawa na makundi ya wakazi ambao waliwatuhumu kuwa walikuwa wanakunywa damu ya binadamu kama sehemu ya tambiko.

Amri ya kutotoka nje usiku imetangazwa na serikali kuzuia vifo zaidi.

Wakazi hawaruhusiwi kutoka nje kuanzia saa moja jioni hadi saa kumi na moja alfajiri.

Wanajeshi wa Umoja wa Mataifa nchini Malawi.

Umoja wa Mataifa umesema kwenye ripoti kwamba uvumi huo huenda ulianzia Msumbiji na kuvuka mpaka hadi kwenye wilaya za mpakani za Mulanje na Phalombe nchini Malawi.

Haijabainika wasiwasi umetokana na nini lakini kwa mujibu wa ripoti ya UN ambayo imenukuliwa na Reuters, wakazi waliweka vizuizi barabarani wakiwawinda “wanyonyaji damu”.

Umoja wa Mataifa uliwaamuru wafanyakazi wake kuhamia maeneo salama kutokana na wasiwasi huo.

Rais wa Malawi Peter Mutharika ameapa kuanzisha uchunguzi kuhusu mauaji hayo na afisi yake imetoa taarifa kwamba suala hilo “limeisikitisha serikali yote”.

Mashirika mengi ya kutoa misaada hufanya kazi nchini Malawi, moja ya nchi maskini zaidi duniani.

Viwango vya elimu ni vya chini mno na maeneo mengi huwa kuna imani za kishirikina.

Msururu mwingine wa mauaji kuhusu wanyonyaji ulikuwa umezuka huko mwaka 2002.

Share this:

  • Click to share on Twitter (Opens in new window)
  • Click to share on Facebook (Opens in new window)
  • Click to share on Google+ (Opens in new window)

Related

Ureno na Ufaransa zafuzu Kombe la Dunia Urusi 2018
Serikali ya wilaya ya SIKONGE kuanza ujenzi wa Madarasa ya kidato cha Tano na Sita.

Related articles

Mabaki ya ndege iliotoweka na…
Refa Mkenya aliyeteuliwa na Fifa…
Rais Madagascar ateuwa waziri mkuu…
Bodi ya usimamizi wa shule…
Mchungaji auawa akiwabatiza waumini Ziwani
Volkano yasabisha vifo vya watu…

Leave a Reply Cancel reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

On Air Now

Download CG Google App here

CLICK TO PLAY CG ONLINE TV

Advertise here

ABOUT US

CG FM RADIO is the radio station that based in Tabora – Tanzania that targets all age groups. Due to its moral observation and ethical programs, CG FM radio continues to have a lot of audience which makes us the best on western zone.

YOU ARE HOME

TWITTER

My Tweets

Menu

  • HOME
  • News
  • Listen Live
  • Advertise