
Watanzania wametakiwa kuwaendeleza wanawake wa vijijini.
Watanzania wametakiwa kuwaendeleza wanawake wa vijijini kwani wao ndiyo wazalishaji wakubwa wa mazao ya chakula na biashara.
Mbunge wa kuteuliwa na mke wa rais wa awamu ya nne Mama SALMA KIKWETE ameyasema hayo katika maadhimisho ya siku ya wanawake duniani ambayo yamefanyika katika viwanja vya CHIPUKIZI Mjini TABORA.
Amesema kuwaendeleza kina mama hao kunasaidia kuweka msingi imara wa maendeleo ya viwanda nchini na usalama wa chakula.
Akisoma Risala muwakilishi wa wajasiriamali Manispaa ya TABORA HADIJA KADONO ameipongeza CG FM kwa kuanzisha CG WOMEN Gala kwani wanawake wamepata elimu ya kudunduliza kupitia kampeni ya kibubu challenge
Mbunge wa URAMBO Mheshimiwa MAGRET SITTA na Mwenyekiti wa wabunge mkoa wa TABORA amezitraka halmashauri zote za wilaya wa mkoa wa TABORA ziwapatie kina mama asilimia nne ili watekeleze adhma ya sera ya viwanda.
Akisoma risala ya wanawake wa mkoa wa TABORA Meneja wa CG FM ambaye pia ni muhamasishaji Mkuu wa tamasha la CG WOMEN GALA mwaka 2018 WINNIFRIDA CELESTINE amesema njia bora ya kumuwezesha mwanamke kiuchumi vinahitajika viwanda vyenye kila zana za uzalishaji ili wanawake waweze kuzalisha bidhaa zenye viwango vya TBS na TFDA ili ziuzwe ndani na nje ya nchi.
Kwa upande wake Mkuu wa Mkoa wa TABORA AGREY MWANRY amemuomba mama SALMA asaidie kuitangaza TABORA kwani kuna fursa za uwekezaji.
Mama SALMA KIKWETE ameiomba serikali kuweka mazingira rafiki kwa watoto wa kike ili wanufaike na elimu kwani takwimu zinzonesha kuwa idadi kubwa ya wanawake wanashindwa kuhitimu masomo yao kutokana na changamoto zinawaozwakabili.
Kauli mbiu ya siku ya wanawake duniani ni kuelekea uchumi wa viwanda,tuimarishe usawa wa jinsia na uwezeshaji wa wanawake vijijini.