
Waumini wa dini ya Kiislamu wametakiwa kufunga siku zote…
Waumini wa dini ya Kiislamu wametakiwa kufunga siku zote za Mwezi Mtukufu wa RAMADHANI kwa kuwani mwezi pekee ambao Mwenyezi Mungu anasamehe dhambi kwa waumini.
Wito huo umetolewa na Shekhe Mkuu wa wilaya ya TABORA,Shekhe RAMADHANI RASHID akisema kuwa Mwislamu atakayefunga na kuzingatia matakwa ya Mwenyezi Mungu katika Mfungo huu wa Mwezi Mtukufu wa RAMADHAN atasamehewa dhambi zake.
Amesema katika kipindi chote cha Mfungo wa Mwezi Mtukufu wa RAMADHAN waislamu wanapaswa kuepuka matendo mabaya ukiwemo uongo kwa sababu ni dhambi kubwa kwa Mwenyezi Mungu.