Skip to content
CGFM
  • Home
  • Listen Live
  • News
  • Presenters
  • Gallery
  • Advertise

Waziri mkuu wa Japan Shinzo Abe ameahidi kukabiliana na…

  • October 23, 2017

Waziri mkuu wa Japan Shinzo Abe ameahidi kukabiliana vilivyo na Korea Kaskazini baada ya matokeo ya kwanza kuonyesha kuwa alipata ushindi mkubwa kwenye uchaguzi wa siku ya Jumapili.

Bw. Abe alikuwa ameitisha uchaguzi wa mapema kwa ahadi ya kukabiliana na changamoto zinazoikabili Japan, likiwemo tisho kutoka Korea Kaskazini.

Vyombo vya habari vinaripoti kuwa muungano wa Bw. Abe umeshinda theluthi mbili ya viti vya bunge.

Hii inampa Bw. Abe nafasi ya kuifanyia mabadiliko katiba ya baada ya vita vya pili vya dunia.

Awali waziri mkuu alikuwa ametoa wito wa kutaka jeshi la nchi lifanyiwe mabadiliko, hatua yenye utata ambayo anasema kuwa inahitajika kuboresha ulinzi wa jeshi la Japan.

Akizungumza baada ya kutolewa matokeo ya kwaza Bw. Abe alisema: “Jinsi nilivyoahidi lengo langu kubwa ni kuikabili Korea Kaskazini.

Miezi miwili tu iliyopita umaarufu wake ulikuwa ukishuka kufuatia kupatikana kwenye sakata, lakini alipata mwamko mpya baada ya Korea Kaskazini kurusha makombora mawili kupitia anga ya Japan.

Vyombo vya habari viliripoti kuwa muungano wa chama tawala cha Abe cha Liberal Democratic Party (LDP) na chama cha Komeito ulishinda viti 312 kati ya viti 465 katika bunge la chini, ushindi unaoupa muungano huo nguvu za kubadilisha katiba..

Awali Bw. Abe alikuwa ametangaza kuwa alikuwa anataka kukifanyia mabadiliko kipengee cha katiba kinachozuia vita na kupelekea kutambuliwa kwa jeshi la Japan.

Miaka miwili iliyopita Bw Abe alifanikiwa kubadilisha katiba ambayo iliruhusu wanajeshi kupigana vita nje hatua ambayo ilipingwa vikali.

Share this:

  • Click to share on Twitter (Opens in new window)
  • Click to share on Facebook (Opens in new window)
  • Click to share on Google+ (Opens in new window)

Related

TABORA: Wauzaji wa dawa na wamiliki wa maduka ya dawa muhimu watakiwa kuzingatia sheria na taratibu za kuuza dawa.
Jitihada za kutokomeza ndoa za utotoni Afrika Magharibi na Kati.

Related articles

Mabaki ya ndege iliotoweka na…
Refa Mkenya aliyeteuliwa na Fifa…
Rais Madagascar ateuwa waziri mkuu…
Bodi ya usimamizi wa shule…
Mchungaji auawa akiwabatiza waumini Ziwani
Volkano yasabisha vifo vya watu…

Leave a Reply Cancel reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

On Air Now

Download CG Google App here

CLICK TO PLAY CG ONLINE TV

Advertise here

ABOUT US

CG FM RADIO is the radio station that based in Tabora – Tanzania that targets all age groups. Due to its moral observation and ethical programs, CG FM radio continues to have a lot of audience which makes us the best on western zone.

YOU ARE HOME

TWITTER

My Tweets

Menu

  • HOME
  • News
  • Listen Live
  • Advertise