YANGA imeondoka mchana wa leo mjini TABORA kwenda SHINYANGA…
YANGA imeondoka mchana wa leo mjini TABORA kwenda SHINYANGA kwa ajili ya mchezo wake ujao wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara dhidi ya wenyeji, STAND UNITED Jumapili, huku huenda wachezaji watatu wakakosa mchzo huo.
Mabeki JUMA ABDUL na KELVIN YONDAN pamoja na kiungo RAPHAEL DAUDI wote walionyeshwa kadi za njano za pili Jumamosi Uwanja wa KAITABA, YANGA ikishinda 2-1 dhidi ya wenyeji KAGERA SUGAR Uwanja wa Kaitaba Bukoba.
Kwa sababu hiyo, watatu hao hawahitaji nyongeza ya kadi kabla ya mchezo dhidi ya mahasimu wa jadi, Simba Oktoba 28, mwaka huu Uwanja wa Taifa mjini Dar es Salaam.
Kuna uwezekano mkubwa, kocha GEORGE LWANDAMINA akawapumzisha wachezaji hao kwenye mechi ya Jumapili kuhofia wasionyeshwe kadi zaidi wakaukosa mchezo muhimu dhidi ya mahasimu.